PATANISHO: Nimemwambia nampenda kwani ni wimbo!

Abigail alituma ujumbe akiomba apatanishwe na bwanake bwana Kipkemboi.

Mzee wangu aliingia nyumbani late hours na nikamuuliza pesa ya maziwa na hapo akaanza kunichapa na hapo nikaenda kwa shemeji yangu kwa siku tatu. Baadaye mamangu akanikujia na tukaelekea nyumbani na tukasuluhisha hayo na nikarudi nyumbani. Alielezea Abigail.

Aliongeza,

Mara ya pili akanitishia kunipiga na hapo nikamwambia kama hataki maneno yangu aniambie niende nyumbani hapo tukabishana na nikaondoka. Singependa mambo mengi na nataka tu kurudi nyumbani tulee watoto wetu.

Kulingana na Abigael wawili hao wamekuwa wakizungumza lakini bwanake humuahidi fedha za nauli lakini hajawahi tuma.

Wawili hao wana watoto watatu katika ndoa ya miaka kumi.

Sasa si nimekubali! Alijibu Kipkemboi pindi tu mkewe alimwomba msamaha.

"Wacha tutaongea naye kwa simu yake kisha nijue siku nitamtumia nauli ili aje." Aliongeza Kipkemboi kabla ya kuthibitisha kuwa anampenda mkewe.

Hata hivyo kulikuwa na kipindi cha ucheshi wakati bwana Kipkemboi alipoambiwa amwambie mkewe maneno ya mwishi matamu kwani alisema, Nimewahi kumuambia nampenda kwani ni wimbo!!

Wololo!