PATANISHO: Nimenyimwa tendo la ndoa na mke wangu

Ikiwa Ijumaa safi, aliyetuma ujumbe leo ni bwana Mike akisema angeomba apatanishwe na mkewe ambaye pamoja wamejaliwa na watoto wawili. Mike anasema wamekosana na tangia mwezi wa nne hajakuwa akila matunda ya ndoa.
Nilioa huyu msichana tangu 2013, nikang'ang'ana na nikampeleka training ya polisi na baada ya mwaka mmoja unusu aliondoka nyumbani na kubeba kila kitu hadi mbuzi.

Anasema kuanzia mwezi wa nne mkewe alikuwa anamnyima tendo la ndoa na isitoshe anamuekea godoro sakafuni ama anamwagiza alale kwenye kiti akisema kuwa amechoka kwa kufanya kazi ya polisi usiku kucha.

Si unajua hii Kenya, nilihongana ili akapata hii kazi ya polisi na tulikuwa tumepanga akimaliza pia mimi niende shuleni nijifunze kuwa mwalimu." Aliongeza.

Hata hivyo pindi tu bi Tracy alipopigiwa simu alikiri kuwa hamjui bwana Mike na aliposikia sauti ya mumewe alisitiza mawasiliano kati yetu na kuzima simu.

Bwana Mike anasema kuwa hajawahi mpiga mkewe na mambo yalikuwa mazuri lakini alikiri kuwa mkewe ashawahi ona picha ya mwanaume mwingine kwa mtandao wa Whatsapp.

Nilipomuuliza kuhusu hayo alini block na kitambo alikuwa anakataa friend request yangu pale Facebook, lakini juzi alimkubali ila tu yeye hawezi tazama kile anachofanya." Aliongeza Mike.

Kulingana na bwana Gidi, bi Tracy alituma ujumbe akisema tayari amepata mume mwingine na hataki kusumbuliwa.