PATANISHO: Nimepoteza watoto wanne kwa sababu ya mama mkwe

Elizabeth mwenye umri wa miaka 24, aliomba apatanishwe na mama mkwe akidai kuwa anataka kujua msimamo wake kwake.

Elizabeth alidai kuwa amepoteza watoto wanne kwa sababu ya mama mkwe kwani alitaka mwanawe aoe msichana mluhya ila sio mkikuu. Anadai kuwa amefikia mwisho.

Nimeolewa kwa familia ya waluhya kwa miaka sita na nimepoteza watoto wanne kuanzia mwaka wa 2015 na Jumanne iliyopita nilipoteza mtoto wa miezi miwili.

Nilikosana na yeye kwani baada ya kifo cha mtoto wa kwanza alidai kuwa mimi ndio nimeua mtoto na hapo nikazungumza maneno machafu, hapo alisema kuwa sitawahi pata mtoto. Alisimulia bi Elizabeth.

Anadai kuwa yeye na bwanake walienda hospitalini lakini walipopimwa hakuna tatizo lolote lilipatikana kwao.

Elizabeth aliongeza akidai kuwa mumewe anampenda na alimuahidi kuwa wawili hao wakitengana hatooa tena na huenda akajitia kitanzi.

Mama mkwe huwa haniambii hapendi wakikuyu lakini yeye huambia watu wengine akisema ana prefer mwanawe aolewe na kabla lake.

Juhudi zetu za kumpata mama mkwe, mama Florence hazikufua dafu.

Je ni mawaidha yepi unayoweza mpa bi Elizabeth?