PATANISHO: Ninakosana na mke wangu kwa ajili na kunywa pombe sana na kutafuna miraa

Katika kitengo cha patanisho Samwel alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe, Sheila baada ya mkewe kulalamika kuwa anakunywa pombe sana na hata kutafuna miraa licha ya kuishi pamoja na mkewe hawaongeleshani.
"Nimeishi na mke wangu kwa miaka miwili na tumebarikiwa na mtoto mmoja, licha ya kuishi pamoja hatuongeleshani. Hii ni baada ya kudai ninakunywa pombe na kutafuna miraa sana

Nimejaribu kujirekebisha na hata kumuomba msamaha lakini hakubali msamaha wangu, nilianza kunywa mwaka wa 2014, kwa sasa si vile nilikuwa ninakunywa kitambo

Nataka kumwambia kuwa sitarudia tena na anisamehe." Alizungumza Samuel.

Sheila naye alikuwa na haya ya kusema,

"Mume wangu anakunywa hata hashughulikii mtoto ata kumnunulia chakula hawezi, nikipata kibarua hataki niende kufanya ilhali haninunulii nguo na chakula

Alinioa nikiwa na mimba vile mtoto amekua anaenda kila mahali akisema kuwa mtoto si wake, nikitaka kwenda kufanya kibarua nipate chakula ananiambia kuwa niende nikaolewe na mtu mwenye naenda kumfanyia kibarua

Nikiwa mgonjwa hawezi nishughulikia, natafuta mtu mwingine afanye kazi awali amekuwa akisema kuwa anataka nimzalie mtoto ilhali mwanangu ana mwaka mmoja na nusu."

Samuel alikiri atabadilika, kwa uhondo zaidi tembelea mtandao wa radiojambo wa youtube.