pata.pata

PATANISHO: Pastor alimdanganya mke wangu eti alimuombea akapata mimba

Hillary ambaye alikiri alikosana na mkewe bi Emily vibaya sana aliomba apatanishwe.

PATANISHO: Mke wangu nimekuwa mchafu tangu uende

“Mke wangu tulijuana mda mrefu, tukapendana tukaskizana. Mimi nilikua naishi Rongai naye Pipeline.” Alisimulia.

Aliendelea;

Sasa tukaskizana tuishi pamoja, wakati niliwacha kazi nikapigwa transfer Mombasa nikaona hapana tumejuana na huyu mtu na hatuja kaa mda mrefu na yeye, siwezi enda Mombasa. Nikakataa nikaamua kuishi naye. 

Kufikia hapo msichana akasema twende kwao nikajua wazazi wake na nikakubali mwezi wa Disemba. Tulipoenda kwao hapo ndipo mikosi ilianza, tukaanza kugombana na kutusiana kwa simu na nikashindwa nini mbaya.

PATANISHO: Niliogopa kuwa mume wangu anaweza niua

Nikarudi Nairobi bila kumwambia. Wakati nilifika nilipata nguo zangu zimetolewa kila mahali na kufichwa chini ya kitanda. Nikamuuliza kwa nini na hakunijibu lakini nashuku kuna pastor anayempotosha.

Pastor anasema eti nitoe pesa elfu kumi eti ng’ombe na mbuzi ndio atuombee ndoa yetu iwe nzuri na nilipokataa tukazidi kugombana. Saa hii bibi yangu ni mja mzito na pastor anaambia bibi yangu eti amemuombea hadi amepata mimba.

Kwa sasa wawili hao hawaishi pamoja kwa mda wa wiki mbili na kila anapompigia simu wanagombana.

Alipopigiwa simu bi Emily alisema kuwa mumewe amekuwa na tabia ya kumkosea na kuomba msamaha kwani kuna maneno kadha wa kadha yalikuwa yanaleta migogoro kati yao.

“Makosa aliyofanya ni makubwa sana siwezi eleza kwa redio kwani pia yeye mwenyewe anajua alichofanya. Kama yeye alikuja kuomba msamaha mbona hajachukua hatua ya kwenda kwa wazazi?” Alimuuliza bwanake.

Skiza uhondo wote.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments