PATANISHO: Pastor Alionesha Mke Wangu Kwa Ndoto Kuwa Nina Mke Mwingine

Martin alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Catherine ambaye alifunganya virago na kuelekea kwao nyumbani.

"Mimi nilikuwa mombasa, sasa mke wangu nilikuwa nimemfungulia kazi maeneo ya Kitui lakini niliporudi nikapata kuwa kuna mambo hafanyi mazuri.

Nilipata vitu nilivyomnunulia alikuwa ameanza kutumia na watu wengine, kwanza nilikuwa nimemshuku kuwa ana uhusiano na mchungaji lakini baadaye nikagundua kuwa hakukuwa na lolote. Sasa nikamweleza kuwa tulifaa tusafiri naye hadi Mombasa lakini akadai kuwa lazima angemuomba mamake ruhusa kabla ya kuondoka nami, na hapo nikamuacha Kitui."

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na nusu na alimuoa mkewe akiwa na watoto wawili.

Martin ana umri wa miaka 40 huku mkewe akiwa na miaka 28.

Alipopigiwa simu bi Catherine alisema kuwa hana hamu yoyote ya kwenda Mombasa kwani kuna mambo kadha wa kadhaa ambayo yanamzuia kufanya uamuzi huo.

"Mume wangu alinikosea sana kwani alinipiga bila sababu yeyote." Alieleza.

"Alinieleza kuwa mchungaji wake alimueleza kuwa ameoneshwa kwa ndoto kuwa nina mke mwingine huko Mombasa, sasa nikaelekea kwa ile kanisa ambayo mke wangu alikuwa amempelekea mbuzi kama jamii ya kwao. Kumbe yule mchungaji akampigia simu mke wangu kudai kuwa nilikuwa namuulizia na hapo mke wangu alianza kudai kuwa nilitishia kumuua mchungaji." Alieleza Martin.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be