PATANISHO: Peninah Amsamehe Patrick Baada Ya Kula Kiapo

patanisho
patanisho
Jumanne asubuhi, wanajambo walishuhudia kisanga kimoja wakti wa kipindi cha patanisho ambapo Jamaa kwa jina, Patrick alipo omba apatanishwe na mkewe Peninah ambaye walikuwa wamekosana masaa ishirini na manne tu. Kisa na maana; Patrick alikuwa amefika nyumbani akiwa amechelewa.

Kulingana na Patrick, alikuwa ameelekea kutizama mechi ya mpira mtaani kwao ambapo alichelewa. Kabla ya kufika nyumbani kwao, rafikiye mmoja alimwomba aelekee kwake ili akawapatanishe yeye na mkewe. Patanisho ndani ya patanisho.

Kisanga hicho kilimchelewesha zaidi Patrick zaidi na pindi tu alipofika nyumbani, mkewe alifunganya virago vyake vyote na kutoweka, licha ya jitihada za mumewe kumwongelesha.

Lakini kisanga kiligeuka baada ya Gidi na Ghost kumpigia Peninah simu na kusimulia kisa tofauti na mumewe.

Peninah alikiri kuwa mumewe ana tabia za kumpiga na kumuumiza licha yake kumpenda na kumvumilia.

Mkewe alisimulia kuwa siku aliyoteweka baada ya mumewe kumwonesha madharau na kutojali kwake. Licha yake kujieleza mbona alitoka alimfuata na kumpiga na isitoshe kumuumiza.

Hayo yalimkasirisha Gidi na kabla ya kuwapatanisha alimuamrisha Patrick ale kiapo cha kutomkosea tena au kumpiga.

Skiza kanda ifuatayo upate uhondo zaidi.

&feature=youtu.be