PATANISHO: Pesa sio shida kwa mume wangu madharau ndio mengi!

Mama Zipporah alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe akisema kuwa amechoka na maisha kwa kuwa amejaribu na ameshindwa.
"Nilipatana na mwanaume Januari mwaka huu na katika harakati ya kupata mchumba nikapatana naye na akaniambia ana bibi na anataka mke wa pili. Nikamwambia sina shida lakini ningetaka kujua kwao naye ajue wazazi wangu." Alisimulia mwanadada.

Aliongeza,

Huyu mwanaume ilipofika wakati wa kwenda kwetu nikagundua ana bibi mwingine ambaye sio yule mke aliyeniambia. Kwanzia hapo uhusiano wetu umeharibika na hataki nifanye kazi yeyote."

Mama Zipporah anasema kuwa mumewe huwa anamlaumu kuwa ana mipango ya kando, mara anazungumza na wanaume wengine lakini hajawahi mfumania.

Hatahivyo licha wawili hao kuwa pamoja kwa miezi saba pekee tayari wana matatizo chungu nzima na kila anapomueleza mumewe watengane

"Pesa sio shida kwake, madharau ndio ako nayo." Alisema mwanadada akidai hataki pesa zake bali uhai tu kwani amemharibia jina lake kwao nyumbani.

Je maisha ya mama Zipporah yalikuwa aje kabla ya kuamua kuolewa?

Tulikaziwa maisha na nilipofikisha umri wa adolescents nikajuana na mwanaume nikapata mimba.

Hatahivyo ilibidi tusitishe patanisho yetu kwani alidai kuwa yule mume wake licha ya kuwa mteja alikuwa anaelekea aliko na ilibidi tumpe nafasi ili azingatie usalama wake.