PATANISHO: Pombe ndio ilinitenganisha na mke wangu

Steve Oduor, 36, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Beryl, 35, ambaye walikosana mwaka uliopita.

"Hatukukosania jambo kubwa ila ni vile nilikuwa nabugia pombe na hapo akasema kuwa nitakapo wacha ndio tutaishi pamoja na hapo akaondoka.

Kabla tuoane mke wangu alijua nabugia pombe lakini nilikuwa napunguza, isitoshe wakati kazi yangu iliisha ndipo nilianza kunywa sana." Aliongeza Steve huku akidai kuwa amewacha pombe kwa mda wa miezi saba.

Wawili hao wameona kwa miaka misaba na wamejaliwa watoto watatu.

"Watu wa kwao nilizungumza nao lakini sioni haja ya kwenda huko kwani sijafanya makosa." Aliongeza Steve baada ya juhudi zetu kumpata Beryl kugonga ukuta.