PATANISHO: Raphael Abubujikwa Na Machozi Baada Ya Mkewe Kutoweka

Raphael alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Veronicah ambaye wameishi kwa miaka saba na pamoja kujaliwa watoto watatu.

"Mimi sijawahai mpiga au kumkataza kutafuta kibarua eneo lolote. Sasa siku moja nilienda kibarua ya kukata nyasi, na kurudi nikapata amefunganya virago vyake na kuondoka.

Jambo hili lilifanyika siku ya Jumamosi na kufanya utafiti hakuenda kwao bali alienda mahala tofauti. Alisema kuwa hatarudi nyumbani kwani alidai mamangu alimgadhabisha kwa maneno aliyosema." Alisema bwana Raphael huku akiongeza kuwa mkewe aliwacha mavazi kadhaa naye akaamua kubeba kila kitu na kumpelekea.

Kulingana na babu yake Veronicah, mkewe Raphael hana shida yoyote naye wala ndoa yake kwani shida kuu ni mama mkwe ambaye ana uzoefu wa kuwahangaisha kila mara.

Shida yake ni kumrushia Veronicah maneno ambayo humpa hofu kuu na hapo akaamua kuondoka na kuelekea nyumbani.

Bwana Raphael alianza kububujikwa na machozi wakati tuliposhindwa kumpata mkewe.

"Sahii nafaa kuelekea kazini lakini sijui namuachia nani watoto wetu." Aliongeza Raphael.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be