gidi na ghost on idd(1)(1)(1)(1)(1)(1)

Patanisho: Samaki tu? Mke afukuzwa na mume wake kwa sababu ya samaki

Katika kipindi chetu cha Patanisho na Gidi na Ghost, bwana mmoja jina lake John alifunguka na kusema kuwa anaomba asaidiwe kumrejesha mke wake nyumbani kwa sababu watoto wao wanateseka.

Jamaa huyu na mke wake,Mama Fortune, walikutana miaka 9 iliyopita na kati ya miaka hizo,binti huyu wamekosana na mume wake zaidi ya mara 11 na amaeenda kwao mara 11.

Kila wakati yeye hurudi kwao wakikosana.

Hata hivyo,mwanamke huyu alipopigiwa simu, alisema kuwa, si yeye alifunga virago vyake  na kuenda bali ni mume wake alimfurusha.

Walipoulizwa kisa na maaana cha kumwambia mke wake hivyo, jamaa huyu alisema walikuwa wamekosana baada ya kumpa mke wake pesa za kuanza biashara ya samaki lakini alipoitishwa pesa za samaki zile na samaki,wakawa na vurugu na mume  wake akaamua kumfukuza.

”Aliniambia ati samaki zangu ziko na dawa, ati nimemwekea dawa na hawezi kula samaki hizi.Ati ata watoto wake hawawezi kula samki nimeleta.”Mama Fortune alisema.

Watu wawili akiwemo mwanafunzi wauwawa na majambazi, Busia

Zaidi ya hayo ilionekana wazi kuwa ni mume huyu  ambaye alikuwa na misukosuko kwani mume wake alianza kusema ni mambo yepi mume huyu  amemfanyia na amini usiamini wengi walisikitika kwani mume huyu amemfanyia makuu.

Mke wake alisema kuwa,bwana John alimshikia panga siku moja na mara kwa mara huwa anamtishia maisha kila wanapo kosana.

Aidha,bwana John huwa anamfuria sana mke wake na ata kukataa kula chake akidai kuwa anawekewa sumu.

Vilevile,bwana huyu alimtusi baba yake msichana ambaye ni mhubiri kuwa yeye huwa anaiba sadaka ya waumini wake.

”Alitusi baba yangu na kusema ati yeye ni mwizi, ati huwa anaiba sadaka.” Mke wake John alisema.

Licha ya hayo, baada ya mazungumzo, mke wake John aliulizwa kama anaweza rudi kwake lakini akasema hawezi labda mpaka mume wake aende kwao akiwa pamoja na ndugu zake waombe msamaha na iwapo wazazi wake watakubali basi atarudi kwa mume wake.

‘Harusi bado ipo!’ Msanii Vivian apasua mbarika

Bwana John aliposikia alichosema mke wake, alisema basi ni heri alee watoto wake mwenyewe kwani hawezi enda kwa kina msichana kwa sababu baba yake alimuonya na kumwambia asiende nyumbani kule.

”Basi kama ni hivyo,si heri nikae pekee yangu nilee watoto wangu kwa sababu baba ya huyu  msichana nilimpigia na amesema nisirudi kwake.Hawanitaki huko.”John alisema.

Hata hivyo, mke wake John alisema kuwa baba yake hakusema kitu kama hicho na kuwa ni yeye mwenyewe alisema hatarudi nyumbani.

Daah!Yalikuwa magumu leo na wakati wa patanisho ulipoisha,Gidi alimuomba bwana John aseme maneno ya mwisho na John kusema kuwa yeye harudi nyumbani na kama bibi huyu hatakubali kurudi nyumbani basi yeye haendi kumchukua.

Mama Fortune naye,alikaza kamba na kusema kuwa, iwapo  mume wake anataka arudi nyumbani ni lazima mume wake afunge safari na kuenda mpaka kwao.

Je mambo ya hawa wawili yatakuaje?

Photo Credits: Amon Mghanga

Read More:

Comments

comments