gidiogidinaghost

PATANISHO: Shiro anataka kumrudia Kamau ‘Mruka mimba’.

Leo katika patanisho  Shiro kutoka Nakuru  aliye na umri wa miaka 34 ametuma ujumbe akitaka kupatanishwa na mpenzi wake Kamau  ambaye ana umri wa miaka 31. Shiro amesema anataka tu kurudiana na Kamau licha ya kwamba  amekataa kukubali mtoto ambaye wamezaa  naye .Hii ni baada ya Kamau kuikataa mimba ya Shiro akisema  siye baba ya mtoto lakini ushahidi na  kila maumbile ya mtoto huyo wa kike yanafanana na Kamau . Shiro amesema ‘ Sitaki alee mtoto,nina  pesa zangu za kulea mtoto’.

PATANISHO: Mume wangu ana uhusiano na wanaume na wanawake!

Kamau alipopigiwa simu amesitasita  na hataki kuzungumza na shiro kwa sababu anadai alimtukana .

Kamau  amedai kwamba Shiro alimtukana  kwa kumwita ‘kihi’. Katika lugha ya  kikuyu ,mtu anayeiitwa ‘Kihi’ ni Yule ambaye hajatahariwa .

Lakini Shiro yuko tayari kulipia vipimo vya DNA ili kuthibitisha kwamba mtoto huyo ni wa Kamau  . Wawili hao wana mengi ambayo yamewatenganisha na mengi yalifichuka  wakati Shiro akizungumza na Gidi na  Ghost baada ya kusema pia kwamba Kamau alikuwa na mke na walikutana wakati mke wa Kamau hakuwepo .

PATANISHO: Mimi staki maneno ya Patanisho kabisa sina huo mda! – Teresa

Jitihada za Gidi kumshawishi Kamau akubali kumsamehe Shiro ili warudiane ziligonga mwamba wakati Kamau alipokata simu kwa mara ya pili lakini mpenzi wake Shiro anasema labda ni kwa sababu mke wake yuko karibu naye . Akihojiwa mbona ametaka sana kurudiana na mume wa mtu ,Shiro amecheka akisema ‘Ni mzuri tu lakini ameharibiwa na wanawake wa facebook’. Ameongeza kusema ‘Hata Kamau aliniblock facebook ati nina rafiki wengi na atapatwa na ulcers’.

Kingine   ambacho Shiro anahisi kimewatenganisha ni uchochezi wa baadhi ya rafiki zake wa kike ambao walimahamisha Kamau kwamba Shiro alikuwa ameolewa huko Thika .Hilo limeonekana kumkwaza sana Kamau ambaye yamkini ameshafanya uamuzi wa kutoendelea na uhusiano huo .Alipoulizwa na Gidi iwapo hamtaki tena Shiro,Kamau alisema

‘ Sitaki Mambo mengi….Simtaki’

Kamau ana umri mdogo kumliko Shiro na hilo pia huenda likawa mojawpao ya sababu zinazoyumbisha uhusiano wao .

Shiro hata hivyo amesimama kidete akisema lazima atamrudia Kamau akisema ‘Sitamwacha hivyo,Nampenda’. Ameahidi kumpigia simu  baadaye ili kumshawishi warudiane .Je,mapenzi yao yataweza kuokolewa?

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments