PATANISHO: Sijaamka na huyu mwanaume ananiharibia moods

William, 36, kutoka Meru alituma ujumbe akiomba apewe fursa amuombe mkewe bi Hilda, 29, msamaha iliwarudiane na walee watoto wao pamoja.
"Tulikosana mwaka uliopita mwezi wa tisa na shida ilikuwa ni nilimkanya asiendanishe na wamama ambao wamevunja maboma yao kwani itasambaratisha ndoa yetu." Alisema Willy.

Aliongeza,

Huyo mama tayari alikuwa amewachana na bwanake na kuondoka na watoto na nilikuwa namkanya kumhusu na dakika ya mwisho yeye ndiye aliyesababisha shida kati yetu. Isitoshe mke wangu aliondoka na kubeba watoto na kila kitu kwa nyumba."

Willy anasema wawili hao huzungumza na yeye hushughulikia watoto wake lakini maswala ya kurudiana bado hayajafua dafu.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka saba.

"Skiza, there is time for everything, wakati wako uliisha na unaniharibia wakati wacha kunisumbua." Alisema Hilda akisisitiza kuwa hajapata mume mwingine ila hayuko tayari kurudiana na Willy.

Aliongeza,

Ana makosa mengi na staki kuzunhumzia ila mwanamke niliyempata naye waendelee kwani nishambariki, nilimfumania ila sikuambiwa. Mimi hata sijaamka usiniharibie mood ya siku."