Gidi na Ghost

PATANISHO: Sijui pesa za mume wangu zinaenda wapi akipokea mshahara

Katika kitengo cha patanisho Bi, Achieng alituma ujumbe ili aweze kufahamu msimamo wa mumewe Simon,katika ndoa yake huku akieleza alisema kuwa mumewe ana wanawake wengi huku akirudi kuwa kijana badala ya kufanya mambo kama baba,mume na mzee wa nyumba.

“Mapema mwaka huu baada ya corona kurekodiwa humu nchini biashara yangu iliharibika na nikaamua kuja kumtembelea mume wangu baada ya kufika nilipata jumbe zake na wanawake wengine

Tulizungumza na kuniambia kuwa atarekebisha tabia yake lakini hajaweza kurekebisha tabia yake, pia endapo atapokea mshahara wake sijui huwa anapeleka wapi

Nikimuuliza hanijibu tumeishi kwa ndoa kwa miaka kumi na saba, na kubarikiwa na watoto wawili, nataka kujua kama mimi niko kwa hesabu ya pesa zake au ni wanawake ambao wako nao peke yake

Kuna siku pia nilimpata na mwanamke.”

Mumewe Simon naye alikuwa na haya ya kujitetea,

“Hao wanawake ni waajiri wangu, na sina mwanamke mwingine yeyote,ni mke wangu ambaye na hofu.”

Photo Credits: radiojambo

Read More:

Comments

comments