PATANISHO: Sina amani kwani mume wangu ana wanawake wengine

Aliyetuma ujumbe hii leo ni mama Sylvia akisema kuwa angeomba kupatanishwa na mumewe bwana Odhiambo huku akidai shida ilianza mwaka uliopita na anasema hadi sahii hana amani moyoni.
"Shida ilianza last year unapata tunakosana tunaskizana kisha tunakosana tena na sijui nini mbaya. Shida ilianza na wanawake kwani hatuishi pamoja kwa sababu ako kazini mbali nami." Alisema Sylvia akiongeza mumewe ni kama hataki waishi pamoja.

Aliongeza,

Amekuwa na mipango ya kando kwa mda na sijakuwa nikishughulika sana. Mwaka wa 2018 nilipojifungua nilienda kumtembelea na nikaona mambi sio mazuri.

Akirudi kwa nyumba simu imezimwa na nikimpigia simu usiku ananitetesha.

Mama Sylvia anasema alipofungua mtandao wa mumewe wa Facebook alipata anazungumza na mwanadada huku wakitumiana jumbe za mapenzi.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka saba na wamejaliwa na watoto wawili.

Alipopigiwa simu bwana Odhiambo alisema kuwa hawezi zungumza na kukatiza mawasiliano kati yetu.