PATANISHO: 'Sisi Kama Wana Marogoli Hatupendi Ujinga, Hatubembelezi Watu'

Bwana Zachary alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mke wa ndugu yake.

"Mimi tulikosana na mke wangu na siku moja mke wangu akapata tukizungumza na dadake na akadai kuwa namtongoza. Mume wa mkwe wangu kabla aage dunia aliniambie kuwa nitunze na niwashughulikie mke na watoto wake, na basi sikuwa na budi ila kufanya hivyo." Alieleza Zachary.

Huyo mwanadada ndiye aliyeanza kunitongoza akisema niwachane na dadake nimchukue ili nimsaidie. Isitoshe kuna vile alikuwa ananitumia ujumbe za kimapenzi mapenzi hivi na nikaambia shemeji wangu amkanye kwani sikutaka yale maneno."

Alieleza akisema kuwa nia yake ni kusaidia watoto wa nduguye.

Alipopigiwa simu bi Everlyn alieleza kuwa bwana Zachary ndiye aliyetaka kumridhi lakini hakutaka maneno yale kamwe.

"Muulize anasaidie aje? Tangu tuzike bwanangu imekuwa miaka mitatu sasa na mtoto sasa ana miaka mitatu, lakini mimi pekee yangu ndiye namshughulikia mtoto."

Wewe ukitaka saidia mtoto lakini mimi apana, mtoto nimehangaika naye kwa kila kitu." Alisema Everlyn.

"Sisi kama wana Marogoli hatupendi ujinga, hatubembelezi watu."

Zachary naye alisema hakutaka kuridhi Everlyn kando na alivyo sema huku akiongeza kuwa nia yake ilikuwa tu kutunza mtoto.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be