PATANISHO: Sitaki Dume Suruali Karibu Nami!

lang'at alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Winnie ambaye walikosana kwa ajili ya tabia zake za kubugia pombe.
"Nilikuwa naonja onja tu kidogo, bibi akakasirika akanikanya na nikaendelea tu kimzaha basi siku moja mimi na marafiki zangu tukabugia, na mke wangu aliponizomea nikampachika kofi moja.Tunapozungumza bibi yangu yuko Eldoret anapoishi na rafiki yake mwingine." Alijieleza Jamaa.

Alipopigiwa simu mama Abby alikiri kuwa tabia za mumewe ndizo zilizomkasirisha kwani amepitia mengi naye na hapo akaamua kutoka na kuelekea nyumbani. "Anatembea na marafiki wadogo ambao hawajaoa na hao ndio wanaompotosha,na kupelekea yeye kusahau majukumu yake." Alisimulia Bi. Winnie.

"Siwezi kaa na mtu ambaye hajui majukumu yake, mtu asiyejua kama yeye ni mwanaume au mwanamke." Winnie alimueleza mumewe huku Lang'at akifichua kuwa marafiki zake humtoroka mara kwa mara na kutokea ifikapo mwisho wa mwezi.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be