PATANISHO: Sitasema kama namtambua Beryl kama mke wangu

Beryl alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Boaz ambaye walikosana na kutengana miezi miwili iliyopita.

"Mimi naona tumekuwa tu poa lakini sarakasi ilianza wakati alichukulia beste yake KDF officer loan. Akaniambia niende nyumbani kwani hangeweza kutushughulikia kwani tuko wake wawili." Alisema Beryl.

Aliongeza:

Nikiwa nyumbani nikapigiwa simu kwamba mtoi anahitajika karo sasa kwa sababu mume wangu alikuwa na madeni nikaamua nitumie TV kama njia ya kulipia deni lile.

Ubaya ni kuwa pia mume wangu alikuwa mgonjwa na alikuwa anahitaji ile televisheni ili aweze kwenda hospitalini, lakini alipopata televisheni haiko alikasirika sana.

Beryl anasema kuwa wapo wanawake wawili kwa hiyo ndoa lakini anashuku kuna wengi.

Wawili hao wamekuwa kwa uhusiano kwa miaka mitatu.

Alipopigiwa simu bwana Boaz, alisema kuwa alivumilia katika ndoa yake na Beryl hata wakati wazazi wake hawakutaka ndoa yao, na licha ya hayo yote Beryl bado anamharibia jina kila mahali anapoenda.

"The problem with you is that you always trust strangers." Alisema Boaz huku akisema mdomo wa mkewe ndio unawagombanisha na hapo ndipo alifika kikomo.

Gidi mimi am an intelligent person na nimefanya investigations zangu na nimejua shida zake." Alijieleza Boaz akisema kuwa hatajibu kama bado Beryl ni mkewe kwani mkewe ana tabia ya kurudia makosa kila siku.

Maneno ya mwisho kwa Beryl?: Aketi chini kwanza afikirie kama anataka hii ndoa au hataki, halafu ana nambari yangu ya simu atanipigia akiamua.

Maneno ya mwisho kwa Boaz?: Amesema nina mdomo ni sawa, naye awache kuskiza maneno ya watu wengine.

&feature=youtu.be