PATANISHO: Siwezi ishi na mke wangu ambaye ni kibeti changu

Bwana Julius aliomba apatanishe na mkewe bi, Sheila au mama Owuor akisema kuwa walikosana mwezi wa Januari, 2019 na tangia siku hiyo hashiki simu zake.
"Madam Sheila mwezi wa nne watoto walipofunga shule, alikuwa anafaa kuja nyumbani na kisha akaniambia kuwa ametahirisha mtoto na hapo shida na mvutano ukaanza.

Nilimuarifu kuwa kama waluhya mtoto anapaswa kutahiri hospitalini lakini awe nyumbani nasi. Tangia hapo yeye husema mara yuko Kisumu mara Mombasa." Alisema Julius.

Wawili hao wamejaliwa watoto wawili lakini mmoja alifariki, katika ndoa ya miaka sita na isitoshe ana mke mkuu.

Nina wake wawili na huyu Sheila ni wa pili na yeye ndiye kibeti changu kwani yeye ndiye anajua mambo mengi. Aliongeza mzee Julius mwenye umri wa miaka 37.

Bi Sheila alipopigiwa simu alisema kuwa yuko kwa mkutano na atampigia mumewe simu ili wazungumze.

Niko kwa mkutano nitazungumza naye baadaye mwendo wa saa sita unusu.

Kabla nimueke kwa nyumba alinipa masharti kuwa lazima mimi na mkewe tuwe sawa, nimnunulie nyumba na nikamnunulia na pia akasema kusiwe na tashwishi kati yake na mke mkuu.

Alinifanya ninunue nyumba kubwa najipikia pekee yangu sio mzuri." Alisema Julius huku akidai kuwa yeye huenda kwa mke mkuu lakini akifikiria kibeti anaumia.

Isitoshe Julius anadai kuwa kuna wapangaji ambao Sheila hakuwa anawapenda na ikabidi awafukuze.