PATANISHO: Heri Nimuue Mke wangu kuliko Nimuone na mwanaume mwingine

Muiruri mwenye umri wa miaka 28, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe, Mary 26, ambaye alikuwa amepanga kumuua na alipofika pale akaamua kujiua lakini yule mke wake akamuokoa.

"Ilikuwa hivi tulikosana mwaka uliopita kisa na sababu ni fedha. Zile fedha nilikuwa nazo nilikuwa nashughulikia shamba fulani nilikuwa nayo Nairobi." Alielea Muiruri.

"Baada ya hayo yote akakubali turudiane na tukaishi pamoja hadi wakati mmoja akaamua kuondoka aniwache, na hapo nikasema kuwa heri nimuue kwani siwezi vumilia kumuona na mwanaume mwingine, lakini nilipofika kwake nikiwa nimejihami na kisu nikashindwa kumuua na hapo nikaamua kujitoa uhai. Nilikuwa nimebeba sumu lakini nilipojaribu kunywa mke wangu akanifungia kwa nyumba vile singeweza kufanya lolote." Alijielezea Muiruri ambaye mkewe yuko Garissa huku yeye akiwa Nairobi ambapo anapokea mawaidha.

Wawili hawa wana mtoto mmoja.

Alipopigiwa simu bi Mary, alikatiza mawasiliano yetu pindi tu aliposikia sauti ya Gidi.

"Kusema ukweli siwezi oa mtu mwingine kwani nimempeleka nyumbani na wazazi wangu wanamjua kwa hivyo inaweza kuwa aibu kuanza kupeleka wengine nyumbani kwa sababu nampenda sana na niko tayari kufa kwa ajili yake. Najua kuna wanawake wengine wazuri lakini siwezi taka mwingine."

"Ananisumbua akili mimi mweleze huvyo kwani nilimpa nafasi afanye anachotaka lakini haskizi. Aendelee na maisha yake na anisahau." Mary alisema baada ya kumpigia simu kwa mara nyingine kabla ya kukata mawasiliano yetu tena.

Pata uhondo zaidi.

&feature=youtu.be