PATANISHO: Tamaa Na Upumbavu Ndio Ulinipelekea Kutafuta Sugar Mummy

Bwana Elly alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Mildred mwenye umri wa miaka 25, baada ya wawili hao ambao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na mitatu, kukosana.

Wawili hao wamejaliwa na watoto, huku mmoja akiwa mlemavu.

Kulingana na Elly, alikuwa na mpango wa kando kwa mda wa mwezi mmoja na tangia mkewe agundue, wawili hao wametengana kwa mda wa miezi minne.

"Nilikuwa na uhusiano na mama mzee ambaye alikuwa wametengana na mzee wake. Ni upumbavu wangu na tamaa ndio ilinipelekea kutafuta mpango wa kando. Ilifika mda nikahamia kwake na nikawaacha mke wangu na watoto wangu. Baada ya mda nikagundua kuwa yule mama huzungumza na mume wake na hapo akaanza kunirushia matusi akiniambia nitoe takataka kwake huku akinitusi na mtoto wetu mlemavu." Alijieleza bwana Elly.

"Babangu amejaribu kumuongelesha mke wangu arudi lakini imeshindikana kwani kila mara husema anahitaji mda wa kutosha ili ajifikirie. Nilimuoa akiwa mdogo sana na mimba ya huyu mtoto mlemavu nilimtunga akiwa shuleni."

Mildred alipopigiwa simu alisema kuwa mumewe amekuwa akimuomba msamaha mara kwa mara lakini alimuahidi kuwa ampe mda afikirie.

"Nilimuambia hizi haraka zake awache, alihama na mavazi yake na kuniacha na watoto na kuelekea kwa huyo mwanamke kwa hivyo nikaamua nibakie tu." Alisimulia Mildred akidai kuwa bado anashikilia kuwa apatiwe mda wa kutosha ili apunguze hasira.

Pata uhondo kamili.