PATANISHO: Tangu nimseti kwa mamake, Mume wangu alihama kitandani

Gidi patanisho
Gidi patanisho
Bi wangui alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bi Njoroge ambaye wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi.

Wangui anasema walikosana siku ya Krisimasi mwaka uliopita akidai kuwa chanzo cha malumbano ni simu ya rununu. Anasema kuwa mumewe hakuwa anajibu simu zake mbele yake.

Tulipanga kwenda Nyahururu krisimasi na tukiwa safarani tukaamua kuingia katika maeneo ya kula na katika juhudi za kula, Njoroge akaitisha kileo. Isitoshe nikama alikuwa anatongoza wale wanadada wa bar na hilo halikunifurahisha.

Aliongeza,

Tuliporudi Kitale maneno aliyo onywa na mamake hakubadilisha na aliendeleza tabia ya kujibu simu usiku wa manane na isitoshe alikasirishwa na kuwa nilimseti.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na bado wanaishi pamoja.

Wangui anasema kuwa mumewe amekuwa na tabia ya kuhanyahanya kwani kuna jirani yake ambaye alitengenezewa simu na Njoroge na hapo yule mwanadada alikuja hadi nyumbani kwake eti kumshukuru. Hapo ndipo uaminifu kati yao ulianza kudidimia.

Isitoshe licha ya wawili hao kuwa pamoja bado wanalala katika vitanda tofauti.

Juhudi za kumfikia Njoroge hazikufua dafu. Je ni mawaidha yepi ungependa kumpa mama Wangui?