PATANISHO: Tayari nishapata mume mwingine kwa hivyo ajisort

Edwin, 33, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Florence, 24, akisema kuwa hakuwa anapenda tabia za mkewe kuenda enda kwao nyumbani kila uchao.

"Alikuwa anaenda nyumbani kila baada ya miezi miwili bila hata kuniambia. Mara ya kwanza alienda nyumbani bila kuniarifu na isitoshe aliwacha watoto." Alieleza Edwin.

"Kesho yake nilimpigia simu nikamweleza kuwa mtoto ni mgonjwa na hakuwa na habari kwani aliwaacha na dadake mdogo. Kumuuliza anarudi nyumbani lini akasema atarudi leo, kukaa kidogo mama akanipigia akisema watoto wamepoteza funguo na wanaumia njaa.

Kupeleleza kumbe alitoka jana yake na kumuuliza alikasirika na kubeba virago vyake. Aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka sita na wamejaliwa watoto watatu.

Tangia watengane mwezi wa Februari wamekuwa wakizungumza na kila wakati mkewe huitisha fedha ili arudi nyumbani, lakini hajawahi rudi.

"Chenye ilifanyika ni eti hatukuwa tunaishi pamoja na yeye alikuwa anapigiwa simu na mamake ambaye alikuwa anamwambia maneno." Alisema Florence huku akisema kuwa tayari amepata bwana mwingine.

Kwa sababu hakuna vyenye anaweza ishi na kahaba na hakuna vyenye anaweza penda mtoto wangu. Mwambie ajisort mimi nishaendelea." Aliongeza.