PATANISHO: Tulikosana na boss wangu kwa ajili ya kifaa cha sh200

Bwana Biwott, 28, alituma ujumbe akisema angependa kupatanishwa na boss wake bwana Waithaka, akidai kuwa walikosana kidogo kwa sababu ya fedha kazini.

"Kuna mahali hatukuskizana kwa pesa kwani kuna kifaa ya plumbing ambacho tulikuwa tununue naye. Yeye ndiye alikuwa anunue lakini ilipofika wakati wa mshahara akasema tutoe zile fedha na hatukuwa tumeelewana vile. " Alisema Biwott.
Kwa upande wake bwana Waithaka alimpa Biwott mawaidha kadhaa akimshauri ajifunze kuskiza maneno anayofunzwa. Isitoshe anasema kile kifaa kilikuwa cha Biwott wala sio chake mwenyewe.

"Nilimwambia hii ni town mtu anafaa kukaa kama mtu amechanuka sio kama wa mashambani huko kwao. Nilikwambia mimi ni kama Uhuru na Ruto tukikaa pamoja." Alisema bwana Waithaka huku akimshauri arudi job mara moja.