PATANISHO: Tulikosana Na Mume Wangu Baada Ya Kukataa Kupimwa Ugonjwa Wa Ukimwi

Jennifer alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana John.

"Tulikosana mwaka wa 2006 wakati nilikuwa na mimba ya kifunga mimba wetu na jamaa wakati huo hakuwa muaminifu. Na hapo nikamwambia twende kliniki kupimwa na nikawa na wasiwasi kwani alikuwa na tabia za usherati kwa sababu nishawahi mpata kwa vyumba vya malazi na wanawake.

Hapo nilimtenga kitandani na nikahama na watoto wetu na hapo akatutenga na watoto kwani ispokuwa kulipa karo hatumi fedha za matumizi.

Bwanangu ana mwanamke mzee huko Kangundo na ningependa arudi nyumbani kwani tulikosania tu mambo ya kupimwa." Alieleza Jennifer ambaye wamekuwa pamoja kwa miaka 17.'

Alipopigiwa simu bwana John alifichua kuwa hajawai funga ndoa kabla ya kukatiza mawasiliano pindi tu jina la Jennifer lilipotajwa.

Pata uhondo kamili.

Bonyeza hapa kwa habari zaidi za

&feature=youtu.be