Patanisho: Tulipeleka mtoto kwa mganga akamnyonya damu, nikatoroka nyumbani

Je ikiwa mme wako anaamini mambo ya mganga baadala ya hospitali una weza mshauri vipi?

Jackie na bwanake walikosana akamwachia mtoto, baada ya kisa cha kuhuzunisha.

Anatuelezea kilichotokea:

'ilikuwa tuu kwa hasira nikawacha mtoto lakini sasa ilifanyika mwezi wa nne. Tulikusana na yeye Januari nikaenda kwetu then nikarudi mwezi wa tatu ikienda kuisha hapo. so huyu mtoto alikuwa mgonjwa wakati tulikuwa pamoja na yeye, wakati tulirudi huyu sasa bwanangu akaniambia kuwa kuna mtu mwenye anaomba na anaweza ombea huyo mtoto apone, so tuka enda na yeye so tulipo fika hapo tukaingia kwa huyo mtu huyo mtu hakukuwa tukaka kakaa then akaniita mimi na mtoto kwa room ingine hivi aka tusurround akachukuwa kitambaa ya red kufunika mimi na mtoto so huyo mwanume akaanza kuomba ameakisha candles kila aina akachukuwa ringi yenye amevaa ya red akaniambia nitoe mtoto tshirt yenye amevaa na akamwekea kwa tumbo akaanza kufinya akatuma baba ya huyu mtoto aende kwa duka anunue wembe akaleta akampea. so mimi nikaanza kutetemeka akaniuliza mbona natetemeka nikamwambia sijawahi amini maombi kama haya na chenye kiko ndani ya roho yangu hakijawahi niruhusu niamini.

so akachukuwa wembe akakata mtoto kidogo then akwa anafinya hiyo ring kwa tumbo akaweka mdomo wake penye amekata na damu. katema damu na hiyo damu ilikuwa na kitu kama glass akaniambia eti hizi vitu ndizo mtoto wako alikuwa ametumiwa. so bwanangu akachukuwa shillingi mia saba akampea, na tukaambiwa kesho yake turudie dawa.

Vile tulienda kwa nyumba tukaanza kubishana akanichapa mbaya sana juu nilimwanbia huyo si mtu wa mungu ni mtu anaabudu madevil na hiyo ni kama sacrifice tulikuwa tunatoa kwa mtoto. 

Wawili hawa waliendelea kubishana hadi mumewe akamtoa nywele, na bibi akatoroka nyumba akihofia maisha yake. Mwezi wa nne ndio ali pigia bwanake simu kumuomba msamaha na warudiane.