PATANISHO: Tuna Watoto Wawili Lakini Bwanangu Hataki Tuongeze Mwingine

John alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Christine akidai kuwa wawili hao walikuwa na ugomvi wa kindoa Ijumaa iliyopita.

"Niliondoka kwelekea kaini na kurudi nyumbani nilipata ameondoka pamoja na mtoto. Nikampigia simu lakini hakuwa anashika na isitoshe sijui kwenye aliko hadi sahii.

Tumekuwa na ugomvi kwani yeye anataka mtoto mwingine na sasa hivi kuna shamba ambalo nang'ang'ana kununua na tayari tuna watoto wawili ambao wametosha."

Alipopigiwa simu bi Christine, "Nilikuwa nataka tu niongeze mwingine na yeye hataki, sasa nilimpata na mtoto mwingine na sasa ni wawili na nilitaka kuongeza wa tatu.

Ukimuuliza anadai kuwa lazima ningoje miaka isonge ili niongeze mwingine. Sasa ilibidi nitoroke." Alijieleza bi Christine huku akiongeza kuwa mumewe amekuwa akihama kwa kitanda chao na swala la kushiriki mapenzi limekuwa shida.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be