PATANISHO: Ujinga wa ulevi ndio ulinitenganisha na mke wangu

Eric na mkewe bi Carol, aliyebeba vitu vyote kwa nyumba na kutoweka mwezi wa Januari tarehe mbili mwaka huu.

"Tarehe 31 Disemba Kuna rafiki yangu aliniitia kamuratina na niliporudi saa kumi na mbili jioni nikapata hayuko na mtoto hana sweta. Kumbe mke wangu alikuwa ameenda."

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka sita na wamejaliwa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka tano unusu.

Alipopigiwa simu bi Carol alisema kuwa Eric alikuwa na tabia ya kumchapa na kumnyonga.

"Hata akitoka kazini alikuwa ananiuliza kwani bado uko kwa nyumba? Hujaondoka?. Isitoshe, alikuwa anapigiwa simu na wanawake simu na anatoka nje hadharani. Kwani mimi sio mwanamke?" Alieleza Carol akiwa na wingi wa hasira.

Carol pia alisema kuwa Eric alikuwa na tabia ya kulala nje na alimngoja kwa miaka sita abadilishe tabia lakini hakubadilika.

Mimi siwezi rudi si ulikuwa unaniuliza nitatoka lini kwa hiyo nyumba? Mpaka unaenda unaambia watu kazini kuwa unanitafutia fare, unadhani sina watu wetu?." Alimuuliza mumewe kabla ya kukatiza mawasiliano.

Carol alisema kuwa kuna mda mamake Eric alitoka nyumbani kuja kumuonya kuhusu tabia zake hadi akashindwa. Alisema shida yake kuu ni ulevi, kupigwa na kulala nje.

"Imagine siwezi rudi hata na dawa, siwezi!" Alisema licha ya Eric kusisitiza kuwa amewacha ulevi.