patanisho.2019

PATANISHO: Ukali wa mke wangu ulinipelekea kubugia pombe

Jacky aliomba apatanishwe na mzee wake bwana Kenbakisema kuwa wawili hao hawaelewani tangia mwaka wa 201 na anahisi kuwa wanaweza tengana wakti wowote sasa.

Jacky anasema wawili hao wamekuwa kwa ndoa tangia 2000.

‘Nitaskuma mswada wa kuhalalisha bangi,’ Mariga aahidi wana Kibra

“Mume wangu anapenda kulewa na madharau tu halafu hadi watoto wanamuogopa kwani wakimuona yuaja wao hukimbia wakimtoroka. Isitoshe akibisha mlango yeye hutaka umfungulie mlango bila kusita, na ukichelewa kiasi ni vita.” Alieleza Jacky.

Aliongeza kuwa kuna wakati pia mumewe alitumia kisu kumpa mwanawe alama mkononi.

Bwana Ken alipopigiwa simu alisema hana ubaya na mkewe na familia yake na isitoshe amewacha pombe.

“Huyu naye ni mkali na nikaingia upande wa ulevi na nikasema kuwa heri nilewe ili nitulie.” Alisema Ken.

Mjue staa wako: Je, Tammy Abraham ni Nani?

Hata hivyo bi Jacky hakutaka kumpa bwana Gidi nafasi amshauri kuhusu jinsi anavyoweza kurekebisha ndoa yake licha ya kuambiwa wazi kuwa ana tabia ya kumkelelesha mumewe ambaye kinyume na mkewe, ni mpole na muungwana.

Ilibidi watangazaji hao wawili wawape wana Jambo nafasi wawashauri wanandoa hawa baada ya kitumbua kuingia mchanga.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments