patanisho Gidi na ghost asubuhi

PATANISHO: Ukiwacha pombe kwa miaka miwili nitarudi kwako

Jamaa kwa jina Kelvin alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Maureen akidai kuwa kuna siku alirudi nyumbani akiwa mlevi na wakapigana.

Asubuhi yake alirudi nyumbani na kupa ameondoka na watoto.

PATANISHO: Mtu akiniita aninunulie pombe nitamshtaki!

“Tulikosana wiki tatu zilizopita na kila ninapojaribu kumpigia tusuluhishe maneno yeye hudai nimpe amani ajifikirie. Alisema Kelvin akidai kuwa shida kuu ni kuwa mkewe hapendi akinywa pombe.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na wamejaliwa watoto watatu.

Huyo story zake za pombe halafu anakuwa violent na kupenda tu vita zaidi. Alisema Maureen akidai kuwa amemvumilia miaka kumi na haoni mabadiliko.

Hapo nikampa mda abadilike na asipobadilike sijui tutakayofanya kwani akinitongoza hakuniambia anapenda pombe lakini tulipopata boma letu akaanza maneno hayo. ” Aliongeza Maureen akidai kuwa mumewe amemzoea sana.

PATANISHO: Bwanangu ana tabia ya kubugia pombe na kunipiga

Kulingana na mkewe Kelvin, atamuamini mumewe akiwacha pombe kwa mda wa miaka miwili na mumewe asiwe na shaka kwani atarudi kwa boma lake.

Isitoshe mumewe ana marafiki wabaya ambao wanampotosha na kumpa mawaidha mabaya.

PATANISHO: Ndoa yangu imesumbuliwa na pombe na marafiki

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments