PATANISHO: Una bibi na watoto mbona unanitafuta?

Bwana Paul alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Esther ambaye walikosana miaka minne sasa.

Alidai kuwa wawili hao wamekuwa wakizungumza licha ya kutengana kwa miaka hiyo yote kabla ya kukata mawasiliano.

Tulikosana baada yake kuskia nina mwanamke nje na wakati walipoketi chini na mamake na kuniuliza kuhusu hayo, nilijipata nikikiri nina mpenzi nje kwani nilikuwa mlevi.

Asubuhi yake mke wangu alikasirika na kufunganya virago vyake na kuondokoa. Nikafanya juhudi za kwenda kwao lakini amekata kurudi kabisa. Alieleza Paul mwenye umri wa miaka 47.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na tisa na tayari wamejaliwa watoto watatu.

Alipopigiwa Esther alishindwa lakusema kwani alishtuka kuwa mumewe alipeleka ujumbe redio Jambo huku akifichua kuwa Paul tayari ana bibi na mtoto.

"Si una bibi na mtoto mbona unataka kumuacha na hawajakukosea? Nilikuambia siwezi ishi na mtu ana bibi wawili." Alieleza Esther.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be