PATANISHO: Unaomba msamaha kwa sababu wewe ni mja mzito na ukijifungua?

Mwanadada alituma ujumbe akisema: Naomba mnipatanishe na mume wangu bwana Ben tulikosana Jumamosi kwa nyumba hatuongei, naitwa Dinah. Nina mimba ya miezi mitano na nilienda hospitalini jana na nikaambiwa nina shida ya pressure.

Ni mgumu sana na ni mtuu wa hasira kuu.

"Kuna msichana alizaa naye mtoto sasa mimi nikampigia simu kumjulia hali, katika hiyo harakati akapigia bwanangu simu akimwambia anikanye kumpigia simu.

Bwanangu kurudi akaniuliza mbona nilimpigia mwenzangu simu na kumtusi na nikajieleza. Katika hiyo harakati bwanangu akakasirika na akaanza kunitusi nami nikamuita malaya.

Isitoshe alisema maneno machungu na akasema kuwa mimi nikama mfanyikazi katika ile nyumba." Alisema bi Dinah.

Alieleza kuwa alikuwa anampigia simu baada ya bwanangu kwanza kumpigia yule mwanadada simu wakipanga kupatana na hilo jambo lilimuuma.

Dinah alikiri kuwa hakumtusi yule mwanadada lakini anasisitika baada ya kumuita mumewe malaya.

Dinah ana miaka 24 huku mzee akiwa na miaka 33, na wawili hao wamekuwa kwa uhusiano wa miaka miwili na huyo ni mtoto wao wa kwanza.

Alipopigiwa simu bwana Ben alisema, Sijui shida yake ni gani kwani akifanya kitu huwa mkali anakuambia maneno mabaya halafu mwishowe akuombe msamaha.

Yaani si mara moja bali ana mazoea.

Licha ya Dinah kuomba msamaha bwana Ben alisema heri tu waachie yote mungu.

Hata wakati nilimuoa hatukumaliza miezi miwili kabla hatujakosana na tunaishi maisha ya kung'ang'ana." Aliongeza Ben huku akisema anampenda Dinah lakini sio kwa asilimia mia kwa mia.

&feature=youtu.be