PATANISHO: "Uza mtoto mmoja upate pesa!" - Stephen

Daisy aliomba apatanishwe na mumewe bwana Stephen huku akitishia kujitoa uhai.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya Miaka 8.

"Mume wangu alikuwa anafanya kazi ya mjengo ambayo alikuwa akimaliza saa kumi na kurudi nyumbani mapema. Sasa ikafika wakati alikuwa anafika saa sita na nilipomuuliza akanipiga vibaya sana hadi nikawekwa chuma mkononi na sasa huwa haufanyi Kazi." Alisimulia.

Aliendelea,

Nikimwambia ashughulikie mtoto anasema niiuze mmoja ili nipate fedha ama nikikosa chakula eti nichinje mmoja tule kama nyama.

Daisy anasema kuwa mumewe alitoweka na kumuachia watoto watatu.

Anasema huwa hawazungumzi na bwabake na hajui aliko kwani mara ya mwisho aliskia uvumi kuwa yuko Uganda. Bwana Stephen alipopigiwa simu alikiri kuwa hamtaki mkewe na alimtenga kitambo.

"Mimi sitaki huyo mtu kwani nina familia yangu. Mimi hao watoto nimekupa kama zawadi yako." Stephen alimfokea Daisy.

Hata hivyo, Stephen, aliahidi kuwa atamtafuta mkewe na kuwashughulikia watoto.