Patanisho ,Vinncent alituma ujumbe wa kupatanishwa na mkewe ambaye wamekuwa kwa ndoa miaka mitatu

NA NICKSON TOSI

Kipindi cha patanisho ni kitengo ambacho lengo kuleta pamoja wote waliokosana kwa jamii ili kupata suluhisho baina yao.

Hii leo katika kipindi hicho, Vinncent wa miaka 30 alituma ujumbe wa kutaka apatanishwe na mkewe Lilly wa 28 ambaye wamekuwa naye kwa ndoa miaka mitatu,Vinncent alidai kuwa licha ya wawili hao kuwa kwa  ndoa kwa muda huo wote ,mkewe anapenda sana mpango wa kando ,swala ambalo lilimpelekea yeye kukosana naye baada ya kufahamu kuwa hakuenda kwao kwa sherehe aliyokuwa amedai anaenda kuhudhuria.

Alipopigiwa simu Vincent alikuwa na  haya ya kusema.

Kuna wakati mke wangu Milicent aliniambia anaenda nyumba kwao kwa sherehe ya kuingiza nyumba,nikanunua bidhaa za nyumbani ili asiende mikono tupu,nilipoamua kufanya uchungu wangu nilibaini kuwa hakuwa ameenda kwao nyumbani bali kwa mpenzi wake wa kitambo,licha ya hayo yotre nimemsamehe na ningepende arejea nyumbani tuendelee na ndoa yetu.alisema Vincent.

Kwa upande wake Lilly alipopigiwa simu alikuwa na haya ya kusema.

Ni ukweli mimi sikwenda kwetu na hii ni kutokana na tabya yake ya kupenda pia mpango wa kando,hata mimi niliamua kuhanya nje ya ndoa na kuamua kurudiana na mpenzi wangu wa zamani,na kila wakati nilipokuwa namuuliza ni kwa nini anaweka picha za wanawake kwa mitandao yake alikuwa ananipa kichapo sana,mimi bado nampenda sana Vinncent.alisema Lilly.

Aidha Vinncent aliposikia kuwa mkewe Llly anatamani kurejea nyumbani alikuwa na haya ya kusema.

Kweli mimi Gidi na Ghost nimefurahia kusikia yeye akisema hivyo kwa kuwa pia mimi nampenda sana,na ningepende tuwache yaliyopita tupange yajayo.alisema Vincent.

Vincent alikuwa na haya ya kuongeza.

Mama Junior kusema kweli nimetembe hii kenya ni nimeona hakuna msichana anaweza vumilia kama wewe,na unafahamu kule tumetoka,nakupenda sana Lilly.alisema Vinncent alipoulizwa amwambie maneno matamu Mkewe Lilly .

Kwa upande wake alipoulizwa Lilly amwambie maneno matamu Vincent,Lilly alikata simu na kudai hawezi sema maneno hayo kwa redio.