PATANISHO: Wacha Aendelee Kulia Mimi Siwezi Rudiana Naye

Baba Lovindia 31, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Lilian, mwenye umri wa miaka 27. Kulingana na jamaa huyo, walikosana na mkewe takriban mwaka mmoja uliopita na alitaka ndoa yake iokolewe.

"Mke wangu yuko kwani ananitafuta tafuta kupitia marafiki zangu ili turudiane. Tulikuwa tunaishi Nairobi na kazi ilipoisha tukarudi nyumbani na bahati nzuri akapata kazi kwa supermarket.

Sasa akaanza kuwasili nyumbani usiku akiwa amechelewa na nilipomuuliza akaanza kuleta maneno maneno. Halafu sasa kuna mwanadada fulani mfanyi kazi mwenza ambaye nikama alikuwa anatongozwa na muhindi ambaye ni muajiri wake na sasa alikuwa anaandamana nao wakienda kujivinjari.

Hapo nikamshauri akiendelea vile pia yeye ataharibu ndoa yake.

Kuna siku mwanadada wa duka la bidhaa za kujenga alinipa nambari yake ya simu ili tuwasiliane, sasa siku moja mke wangu akachukua simu yangu na kumpigia mwanadada yule simu huku akimtusi na kwa hasira nikamzaba kofi hapo ndipo alipofunganya virago vyake na kuondoka."

Wawili hao wana mtoto mmoja wa kijana.

Alipopigiwa simu bi Lilian, "Aii mimi siwezi rudiana naye kabisa nilishaendelea na maisha yangu, sijapata mume mwingine lakini simtaki." Alisema.

Kulikuwa na maneno mengi ya kifamilia, kwa mfano ana tabia za kunywa pombe, kunipiga. Nilikuwa na kazi na sasa imeisha kwani fedha zote ninazompa za kufungua biashara yeye anazitumia kwenda kunywa na kujivinjari na wanawake." Aliendelea kabla ya bwana Edwin kukana madai yote.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be