patanisho new

PATANISHO: Wacha nifikirie kwani nikirudi kwako tena utaniua – Jacky

James aliomba apatanishwe na mkewe akidai walikosana na bi Jacqueline tarehe sita mwezi huu na akaondoka.

“Tulikuwa tumekosana kitu wiki moja iliyopita na nikamchapa kwa sababu ya kumtusi. Tukaketi chini na tukazungumza na hayo yote yakaisha. Sasa sijui kilichotendeka kwani nilienda kazini kurudi nyumbani nikapata ameondoka.” Alieleza James.

Ruto hachelei! amrejeshea Raila makombora ya siasa za katiba

James anadai vita vyao vilianza baada yake kumuuliza kitu alichojua na mkewe akakasirika na kumtusi vibaya maneno ambayo hawezi taja hewani.

Anadai mkewe amekodisha nyumba hapa tu town na juhudi zake za kumtafuta zilipelekea mkewe kutaka kuanzisha matusi tena na hapo akaondokea mazungumzo yao.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka 11 na wana watoto wawili huku kifungua mimba akiwa kidato cha kwanza na kitinda mimba akiwa darasa la tatu.

“Wacha kwanza nifikirie ulichofanya mimi siwezi rudi kwako sahii, wacha kwanza ni relax akili.” Jacqueline alimuambia mumewe.

“Kuna makosa mengine alifanya na siwezi msamehe, alinigonga tumbo nikaanza kutoa damu na hadi wa leo haijawahi wacha. Amekuwa akinipiga naondoka narudi lakini sasa ikaja ikawa mbaya.

Pesa Otas! Vihiga United yasajili wachezaji 10 wapya

Nataka kutulia nikifikiria kama nitaondoka au nitabaki. Aliongeza Jackie akidai kuwa bwana James alisema kuwa aliwahi tishia kutolipia watoto karo ya shule.

Aliongeza akisema, wacha kwanza nipone kwani nikirudi wakati mwingine nikuniua utaniua.

Orodha ya Marais na mitindo ya nyimbo wazipendazo

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments