PATANISHO: Wambui aomba kulea wanawe baada ya kumpoteza kifungua mimba

Ambrose, 45, na mkewe mama Peter, 38, akidai kuwa wao ni wazazi wa watoto watatu na juzi walimzika kifungua mimba na angetaka wazungumze kuhusu watoto waliobaki.

"Mke wangu alienda mwezi wa tano tarehe moja. Mtoto mwenye umri wa miaka 20, alijitoa uhai kwa kunywa sumu kwa sababu ya tofauti yangu na mamake, nilijua kwa sababu alikuwa ametorokea kwa ndugu yangu." Alisema Ambrose.

Kulingana na jamaa huyu, mkewe alikuwa ametoka nyumbani kwa mda wa miaka minane na aliporudi alikaa miezi tisa pekee kabla ya kutoweka tena.

"Nilikuwa nataka tumalize tofauti baina yetu kwani hata tayari amechukua mtoto mwingine. Nilifanya na makosa na nikafanya urafiki na madam mmoja na tukazaa mtoto mmoja kabla yake kurudi kwao." Aliongeza.

Wawili hawa wamekuwa kwa ndoa ya miaka 23.

"Mimi Mwangi nilikusamehe lakini kuishi nawe ni ngumu kwani nina uchungu kuhusu mtoto wangu. Nipatie watoto wangu nitawalea siwezi kuzuia watoto wako." Alisema bi Wambui akimsihi mumewe.

Mwambie afungue simu na kama ni mtoto anataka nitampatia kwani hata alimtoa shuleni." Alijibu Ambrose