PATANISHO: 'Wanaume tuliumbwa ili tuteseke,' - Edwin

patanisho kuteseka
patanisho kuteseka
Edwin 38, aliomba apatanishwe na mkewe wa miaka 16 akisema haelewi aliko kwani alitoka na kwenda na watoto huku akiwacha barua.
Kawaida nilitoka asubuhi wiki iliyopita nikielekea kazini. Mke wangu alikuwa ameniambia nimwachie 300 nikamwambia Nina 250 lakini nitamuachia 200 nibaki na 50 ya nauli. Sasa akateta lakini nikamwambia nitamtumia nikifika kazini ikiwa nitafanikiwa.

Anasema jioni alirudi akiwa amechelewa na alimpata nyumbani na hakuwa anamuongelesha. Alimweleza hakufanikiwa kupata fedha na asubuhi yake akachukua Ile 200. Kurudi jioni alipata mkewe ameondoka huku akiwa amewacha kijibarua kilichoandikwa,

"Nimeenda ukijiskia unaeza nitafuta na usipojiskia ni sawa ntarudi nikitaka."

Kumpigia simu alisema yuko tu Kenya.

Janet alipopigiwa simu alikuwa na haya ya kusema,

Nilimuomba fedha juu niko kwa chama fulani. Sikuwa nazo na alisema hana fedha, mara ana 200 mara 250 na nilishindwa kuelewa.

Edwin alimbembeleza mkewe arudi nyumbani akisema baridi imekuwa nyingi kwa nyumba na amejaribu blanketi na hazitoshi.

Janet naye alimpa usshauri akisema,

kama baridi ni nyingi oga maji moto na ujifunike na blanketi tatu.

Wacha nitulie Kwanza Kisha ntarudi. Unajua ukipenda mtu hufika mahali anabadilika, lakini nampenda hakuna mwanaume mwingine Napenda kwani yeye ndiye baba ya watoto wangu.

Janet alishangaza wengi aliposema kuwa yuko tu karibu na mumewe na huwa anamuona kila siku.

Janet alimpa Edwin hakikisho kuwa atarudi nyumbani siku ya jumapili lakini alimpa masharti ili waweze kuendeleza maisha yao.