PATANISHO: Wazungu wanasema never rattle a snake!

Phyllis alituma ujumbe akisema kuwa angependa kupatanishwa na mumewe kwani alitoka kwa nyumba baada ya wifi wake kumpiga na mumewe hakuwa karibu na isitoshe mumewe amekataa kuja wazungumze.
"Ilikuwa mwezi wa nne na tukakosana na shemeji yangu kidogo na akaja mpaka kwa boma langu, tukatusiana naye na mzee alikuwa. Mzee aalimfukuza na akaenda baada ya kuvutana sana." Alisema.

Aliongeza akisema,

Mzee aliporudi shuleni dadake akaapa kuwa atakuwa ananipiga na kuna mahali tulikuwa tunaenda sherehe na kuna mahali tulikuwa tunashona nguo. Mumewe yule mwanadada akaniambia nipitie kwake nichukue fedha ili niendee nguo zake.

Nikiwa mle nje nikingoja fedha yule shemeji akaja akanitandika na hapo nikatoroka na kwenda zangu.

Kulingana na Phyllis mumewe alimwambia kuwa anafaa arudi nyumbani kwani sio yeye alimkosea na licha ya hayo yule mwanadada bado anaapa kumpiga.

Anasema kuwa yule mwanadada nikama anataka kumfinyilia afanye anachotaka na ana mambo mengi.

Nasema hivi, sio mimi nilimkosea kwani nilirudi nyumbani na nikapata mke na watoto hawako. Nimekuwa nikimtumia fare arudi na hajawahi rudi na nashindwa shida yangu ni gani.

Alisema mzee akidai kuwa wazungu walisema 'Never rattle a snake' akimaanisha kuwa ndiye anamkosea wifi wake heshima.