Patanisho: Aliambiwa kuwa mimi navuta bangi kisha akenda kwao

Bwana Jared aliomba apatanishwe na mkewe Grace baada ya ndoa ya wawili hao kuvunjika mwezi Mwachi mwaka huu wakati Mama Ariet alipofunganya virago vyake na kurejea kwao kufuatia madai kuwa Jared alikuwa mlaguzi wa bangi.

"Nilikuwa nalewa na kurudi nyumbani saa mbili usiku. Nilikuwa naingia kazini saa kumi na mbili asubuhi na kutoka saa mbili usiku jambo lilofanya nikose wakati wa kushiriki na mke wangu. Mama Ariet nilimwoa akiwa na mtoto na ndoa yetu ilidumu kwa muda wa miezi sita pekee. Hata hivyo, aliambiwa kuwa mimi nilikuwa navuta bangi na marafiki zake na akakubali kisha akenda kwao."

Mama Ariet ambaye aliolewa akiwa na mtoto mmoja alisema kuwa mumewe alikuwa na mazoea ya kulewa sana hivyo yeye aliamua kumwacha aendele na pombe yake.

"Najua kuwa alikuwa anatumia mihadarati.Na mimi nilimwonya akakataa kuniskia sasa nikamwacha. Alikuja kwetu akambiwa na wazazi wangu ila akasema yeye atazidi kukunywa busaa."

Mama Ariet alikataa kumrudia baba ariet na kusema kuwa ameendelea na maisha yake.

"Mimi nimerudi kwa bwanagu wa kwanza na hivo nimeshaolewa. Jared endelea na mambo yako kwa sababu mimi nimekusahau kwa sasa."

"Haya ni magumu ila ningependa ufikirie tena kwa sababu mimi bado nakupenda sana na hata miaka kumi ijayo bado ntakuwa nakupenda," Jared alisema baada ya mama Ariet kusema kuwa hawezi kurudi kwake na tena kuongeza kuwa alikuwa amerudiana na babaye Ariet tena.