logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa aachwa kwa kutoshika simu za mkewe

Murigi alisema mkewe alilalamika kuhusu yeye kutochukua simu zake wakati akiwa kazini.

image
na SAMUEL MAINAjournalist

Patanisho17 October 2024 - 08:38

Muhtasari


  • Murigi alisema ndoa yake ya miaka miwili ilisambaratika wiki jana baada ya kutofautiana na mkewe kuhusu suala la simu.

Dennis Murigi ,24, kutoka Nyeri alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Emily Mukami ,20, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Murigi alisema ndoa yake ya miaka miwili ilisambaratika wiki jana baada ya kutofautiana na mkewe kuhusu suala la simu.

Alisema mkewe alilalamika kuhusu yeye kutochukua simu zake wakati akiwa kazini.

"Mke wangu alikuwa ananipigia simu nakosa kupokea. Wakati mwingine nakuwa bize. Nafanya kazi nakosa muda wa kuchukua simu. Nilijaribu kumweleza mke wangu akauliza kwa nini nakuwa bize kila wakati. Wakati napata muda usiku napata ashalala. Nimeongea na yeye akasema nimpatie muda afikirie," Murigi alisema.

"Sijapigia watu wa kwao. Huwa naskia Patanisho ndiyo poa," aliongeza.

Juhudi za kumpatanisha Murigi na mkewe hata hivyo hazikufua dafu kwani Bi Mukami hakushika simu yake alipopigiwa.

Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved