gidi

Patanisho:Daah! Wapenzi wakosana na kukata uhusiano baada ya miaka 17

Hivi leo katika kitengo cha patanisho,bwana mmoja, Justus alitaka Gidi na Ghost kumsaidia kumrejesha mke waliokuwa wamekosana mwaka 2017. Alisema licha mkewe kwenda alikuwa  bado anampenda na alitaka sana arudi nyumbani.

Wapenzi hawa walikaa katika ndoa kwa miaka 17 na pamoja wana watoto watatu ambao huishi na baba yao.

Ilikuaje: Cyrus Ng’ang’a azungumzia ubunifu uliompa hadhi duniani kote

Mkewe alipopigiwa simu alizungumza kwa hasira na machungu akisema kuwa, hawezi kurudi tena kwa nyumba ya Justus kwa sababu baada ya kukosana mumewe alikataa kwenda kuona wakweze ili watatuwe mambo.

 

Zaidi ya hayo, mama huyu alisema kuwa, bwanake hajawahi kumlipia mahari na hata walipokosana mume wake hakuona maana ya kwenda kwao.

”Huyu mwanamume hajawahi ona wazazi wangu, hata mahari hajalipa na hata alikataa kwenda kuona wazazi wangu.” Mama huyo alifoka.

“Uso wangu ulikuwa kama nyama ilioteketezwa,” – Kelvin Kairo

 Mwishowe, alisema kuwa hataki kuanikwa kwa radio tena na kushikilia msimamo kuwa kamwe  harudi tena kwa mume wake.

Je Justus atafanya nini?

 

 

Photo Credits: Amon Maghanga

Read More:

Comments

comments