IMG_9952

Patanisho:”Hii ndio siku ya mwisho nakuongelesha.”Bwana amuambia mke wake

Hivi leo katika kitengo cha patanisho,ilikuwa ni wazi kuwa, wakati mwingine chombo kikienda mrama huwezi kirejesha mkondoni.

Patanisho ya leo ilishindikana kwa sababu wapenzi hawa wote hawakuwa tayari kuridhiana na walikuwa na misimamo migumu.

Hakuna ambaye alikuwa anataka kuomba msamaha na kurudiana na mpenzi wake hata baada ya kuishi kwenye ndoa kwa miaka 10.

Betty Bayo aeleza mahangaiko YouTube, sifa za Victor Kanyari kwake

Wakati mwanamume alituma ujumbe wa kuomba apatanishwe na mamake watoto wake hakuonyesha kuridhia matendo yake yaliopelekea wao kuachana.

”Mpigieni huyu nijue msimamo wake kama atarudi ama nijipange ”Bwana aliandika.

Bwana alisema pia, kilichomtengenisha na mkewe ni mambo ya kinyumbani na kudai kuwa sababu kuu ilikuwa mkewe kuwapiga watoto kila mara na kupiga kelele nyumbani.

Mama watoto alipopigiwa simu alikuwa na msimamo mkali na kusema kuwa hawezi rudi tena kwenye nyumba ya jamaa huyu kutokana na madharau yake.

”Siwezi rudi mimi,heri nilee watoto wangu mwenyewe na nitafute kazi lakini siwezi rudi huko. Bwana anasema ati niliua mtoto wake?”Bibi alisema.

Maisha ya huntha! changamoto za kuwa na sehemu mbili za siri

Mume wake naye hakuonyesha nia ya kumwomba msamaha vizuri, alisema wazi kuwa ni sawa vile ambavyo mke wake ameamua na leo ni siku ya mwisho anaongea naye.

”Leo ni siku ya mwisho tunaongea na wewe,nakutakia heri.Ni vile umeamua sasa siwezi fanya kitu.”Bwana alisema.

Mke naye alipoambiwa aseme maneno yake ya mwisho alisema kuwa, ni kweli yeye harudi huko na ni heri mume huyu atafute mke mwengine.

 

Photo Credits: Amon Maghanga

Read More:

Comments

comments