IMG_9946

Patanisho:Je atakula kiapo?Binti auza uhusiano wake na mpango wa kando

Leo katika patanisho, binti mmoja jina lake Nelima alifunguka mwanzo mwisho na kusema kuwa alimkosea mume wake na anaomba apatanishwe naye.

Amini usiamini,binti huyu aliweka picha za mpango wa kando kwenye mtandao wa kijamii, mume wake akaziona na kusitisha uhusiano wao.

Wanaume wa Lamu wahimizwa kuendelea kuzaa na wake zao

Gidi na Ghost walipompigia simu mumewe Nelima, alishika simu na Nelima akaambiwa amuombe msamaha.

Bila kusita, Nelima alimuomba mume wake msamaha kwani alijua fika kuwa alimkosea sana.

Aisee! kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa, mume wake Nelima alipigiwa simu na kusema kuwa, anaweza kumsamehea lakini hofu ni kuwa anaogopa mke wake anaweza rudia makosa yale.

Wakati umefika!Jacque Maribe aonyesha sura ya baba ya mtoto wake

”Mimi Nelima nitakusamehea lakini shida sasa ni kama utarudia tena.Ukirudia tena sitaongea kitu chochote.” Mume wake alisema.

Nelima aliapa kutorudia kosa lile.

Vilevile, Gidi na Ghost walimlazimu ale kiapo na akatii amri.

Mwisho kabisa, wapenzi hawa walipatanishwa na kuambiana maneno matamu.

Ama kwa hakika,mapenzi kikohozi ukificha chozi lasaliti.

 

 

 

Photo Credits: Amon Maghanga

Read More:

Comments

comments