Gidi na Ghost

PATANISHO:Mke wangu aliniacha baada ya kushuku nina uhusiano na mpishi

Bwana Mugaka alituma ujumbe apatanishwe na mkewe, Kwamboka ambaye walikosana naye miezi sita iliyopita baada ya mkewe kumshuku ana uhusiano wa kimapenzi na mpishi alipokuwa anafanya kazi.

“Mke wangu aliniacha baada ya kunishuku nina uhusiano wa kimapenzi na mpishi wa kazini, hii ni baada ya mpishi huyo kunipigia simu kila siku na kuniuliza kama nimefika salama

Wakati mmoja alipiga simu mke wangu akapokea, mwanamke huyo alimuuliza kwani yeye ni nani kwangu, kesho yake nilipoenda kazini kurudi nilipata amekusanya virago na kuenda.” Alieleza mwanamume huyo.

Kwamboka naye alikuwa na haya ya kusema,

“Mimi nimemsamehe lakini anapaswa kurekebisha tabia yake, si kumshuku lakini nilimpata na mwanamke mwingine, amekuwa na wanawake wengi ilhali mimi ni bibi yake 

Alikuwa anaenda ata kulala nje kwa wanawake.” Alieleza Kwamboka.

Photo Credits: radiojambo

Read More:

Comments

comments