PATANISHO:Nilikosana na mke wangu baada ya kutaka simu yake nichukue mkopo

Leo katika kitengo cha patanisho Fred alituma ujumbe ili apanishwe na mkewe Terry waliokosana Machi mwaka huu baada ya kutaka kuchukua simu ya mkewe ili aweze kukopa pesa.
"Nilikuwa nimechukua simu ya mke wangu ili nikope pesa nimlipie mtoto karo ya shule kwa maana alikuwa ametumwa nyumbani alafu mkopo huo nilikuwa nataka kulipa deni ya pikipiki yangu

Mke wangu alikataa, nilimueleza kuwa ni mimi nitalipa deni hilo ilhali alikana, nilichukua laini ya simu na kwenda nayo kazini

Niliporudi kwa nyumba jioni aliniambia kuwa anataka kwenda, mimi nilifikiri ni mzaha nikamwambia anaweza kwenda lakini haikuwa mzaha alienda sasa anaishi na mama yake Nairobi." Alieleza Fred.

Terry naye alikuwa na haya ya kusema,

"Mimi na mwanamume  huyo hatuna kitu cha kuzungumza, mimi nishaaendelea na maisha yangu, tayari nina mume mwingine nilimpenda sana ilhali alikuwa ananichezea

Tafadhali aweze kuendelea na maisha yake vile nimeendelea na yangu."

Fred alikubali uamuzi wa mkewe na kisha kusema kuwa hawezi pata mwanamume mwingine wa kumuoa.

Je utampa ushauri upi Fred?