PATANISHO:Nilimpa rafiki yangu gari la mwajiri wangu ili afurahishe mpenzi wake

Leo hii katika kitengo cha patanisho bwana odinda alituma ujume apatanishwe na mwajiri wake ambaye waliokasana naye wiki jana, hii ni baada ya odinga kumpa rafikiye gari la mwajiri wake na mwishowe mwajiei wake akamuona nayo.

Akieleza jinsi alivutwa kazi alikuwa na haya ya kusema;

"Nilimpa rafiki yangu gari la mwjiri wangu ambali ni la texi ili aweze kumfurahisha mpenzi wake, mambo hayakuenda vyema kwa sababu baada ya kumpa alionekana na mwajiri wangu na kisha akachukua pikipiki na kumfuata

Alipowashika aliwashukisha rafiki yangu na msichana wake kwenye gari aliponipigia simu nilimwambia kwamba niko shughuli za kikazi

nataka nimuombe msamaha ili aweze nirudisha kazi, tangu hiyo siku sijui huyo jamaa alielenda wapi wala kama yuko na huyo msichana." Alieleza bwana huyo.

Mwajiri wake bwana Sylvester lipopigiwa simu naye alikuwa na haya ya kueleza kuhusu kesi hiyo.

"Huyu jamaa nimemuoonya mara nyingi sana awache kucheza na kazi lakini hakusikia kwa mara ya kwanza aliwapa marafiki zake gari nilipomuuliza aliniambia tu yuko kazini lakini nilikuwa nimeona gari langu likiwa na wasichana

Aliporudisha gari nilimuuliza na kumsamehe, sasa mara ya pili alimpa rafiiki yake na nikaenda kuwashukisha katika gari langu

wacha kwanza atulie ajue maana ya kwanza nikifikiria tena naweza muita." Alisema Bwana Sylvester.

Je kama wewe mwajiriwa na mwajiri ushawahi pitia kitendo kaa hiki na ulifanya suluhu gani ili kusikizana na mwajiei au mwajiriwa wako?