Patashika yazuka baada ya maafisa wa EACC kuvamia afisi ya Sonko

sonko
sonko
Kumezuka patashika  siku ya Jumanne wakati maafisa kutoka tume ya Eacc  walipovamia  afisi ya kibinafsi ya gavana wa Nairobi Mike Sonko katika eneo la Upper Hill .

Maafisa kadhaa wa polisi walikuwa wamendamana na makachero kutoka Eacc  katika afisi ya gavana huyo  iliyojengwa kwenye kipande cha ardhi yenye thamani ya shilingi milioni 500 ya wafanyikazi wastaafu wa  Kenya.

Polisi walikuwa wamekuja kukadiria thamani ya kipande hicho cha ardhi, thamani yake inakadiriwa kuwa shilingi  milioni 500.

Hata hivyo maafisa hao walipofika walizuiwa kuingia na wafuasi wa Sonko  na wakalazimika kukwea lango kuu ili kuingia ndani ya jengo hilo.

Baada ya takriban saa tatu za mshikeshike, maafisa hao waliondoka bila kutekeleza walicholenga . EACC inachunguza jinsi Sonko alivyopata ardhi hiyo .