PATIKANA: Bastola aliyotumia Babu Owino kumpiga risasi DJ Yapatikana

Babu Owino akiwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani
Babu Owino akiwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani
Bastola ya mbunge wa Embakasi Mashariki  Babu Owino  ndio iliyotumiwa katika kisa cha  ufyatulianaji risasi na kusababisha kujeruhiwa kwa mtu mmoja katika eneo la burudani la B Club ,Polisi wamesema . Mkuu wa polisi wa Kilimani Lucas Ogara  amethibitisha hilo akisema mwathiriwa yupo katika hali thabiti . “ Hatuwezi kutaja jina la mwathiriwa kwa sababu ni kinyume cha sheria . lakini tumepokea ripoti kwamba risasi ilipitia shingoni mwake’. Ogara amesema .

Ogara amesema wanamzuilia Owino katika kituo hicho  nab ado hajaandikisha taarifa .DCI imesema imapata risasi tisa na ganda moja la risasi  katika eneo la tukio ."... Vyote vimewekwa kama ushahidi  na vitachunguzwa na watalaam wa bunduki’  mkurugenzi wa DCI  George Kinoti amesema .

https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1218112033025077250?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1218112033025077250&ref_url=https%3A%2F%2Fwww.the-star.co.ke%2Fnews%2F2020-01-17-babu-owinos-gun-used-in-kilimani-shooting-police%2F

Awali wakili wa Babu Cliff Ombeta amesema mteja wake alikaribiwa kwa njia ya kimabavu na  mtu aliyemdhani kuwa rafiki yake na kusababisha  purukushani . Amethibitisha kwamba  bunduki ya Babu sasa  imechukuliwa na polisi na  mbunge huyo ana leseni yakuwa na bunduki . Wakili wake amesema tukio hilo sio la mauaji kwani mwathiriwa yungali anapokea matibabu hospitalini .