Patrice Evra atangaza kustaafu kwake baada ya miaka 20

Aliyekuwa mlinzi wa Manchester United na Juventus Patrice Evra ametangaza kustaafu kwake kutoka soka ya kulipwa akiwa na umri wa miaka 38. Evra ambaye ni raia wa kifaransa aliyezaliwa nchini Senegal anakumbukwa kwa kasi yake ya ajabu pamoja na uongozi wake ndani ya Uwanja.

Evra alichezea Klbau ya Manchester United kwa miaka nane kuanzia mwaka 2006 hadi 2014 ambapo alishinda mataji 10 kwa pamoja. Evra alijiunga na klabu ya Juventus msimu uliofuata huku akishinda mataji mawili na waitaliano hao.

Msimu wa 2016/2017 Evra alijiunga na Mersaille ya ufaransa kwa msimu mmoja kabla ya kumaliza taaluma yake na klabu ya West Ham ya Uingereza.

Evra aliwakilisha taifa lake la Ufaransa mara 81 ndani ya miaka 20 ya kisoka.

Kwa sasa, Evra anatarajiwa kuendeleza elimu yake ya kuwa kocha na huenda akaanza taaluma yake rasmi ndani ya miaka miwili ijayo.